GET /api/v0.1/hansard/entries/1291714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291714,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291714/?format=api",
    "text_counter": 357,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Murgor",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Sisi kama viongozi ndio tutakaoleta suluhu na kuelekeza watu wakae kwa njia inayofaa. Serikali imetuma vikosi North Rift kutafuta suluhu na kuleta maendeleo ili wawache kuzozana, wakae pamoja na kugawa rasilimali pamoja. Kaunti ya Turkana ina sehemu ya kati ambayo haina shida za vita kwa sababu hakuna kinachoendelea. Pahali kuna shida ni kwenye mipaka. Mbona Turkana ya Kati haiendelei? Non-governmental Organizations (NGOs) zimejaa katika Kaunti ya Turkana. Hakuna kaunti iliyo na NGOs nyingi kama Kaunti ya Turkana na hakuna maendeleo. Shule ni za undongo na mahospitali haijafika kwenye kiwango Waturkana wangependa kwani hakuna madawa. Mambo ya irrigation haijaafiki. Kitu gani ambacho kinachukua rasilimali ambazo zinaenda katika Kaunti ya Turkana. Mbali na Kaunti ya Nairobi, Turkana ni ya pili kupata mgao wa kaunti wa juu."
}