GET /api/v0.1/hansard/entries/1291840/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291840,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291840/?format=api",
    "text_counter": 483,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13583,
        "legal_name": "Chute Mohamed Said",
        "slug": "chute-mohamed-said"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, walisema kuna watu wanaitwa “ Wajakoya” waliofika huko na kuokoa maisha ya watu wetu. Nikawauliza Wajakoya ni akina nani. Wakaniambia, hao ni askari jeshi ambao Mhe. Rais Ruto alipeleka kule Samburu, mahali panaitwa Baragoi. Watu wameanza kupata maisha mazuri na kulala vizuri. Kwa hivyo, siwezi kubali mtu yeyote akisema kuna shida ni kuwa Mhe. Rais Ruto hajashugulika. Kule nimetoka Marsabit, tulikua na shida kubwa sana. Kule Sondu watu wamefariki. Mambo haya siyo rahisi. Ningependa kusema pole kwa familia hizo. Lakini ukiangalia hapa nchini, mahali kama Marsabit, watu wengi wamefariki sana na ni zaidi ya mia tano. Wako na watoto, kina baba na mama na familia kubwa sana. Bw. Spika, Mhe. (Prof.) Kindiki amepunguza shida ya Marsabit. Leo ile shida imebaki ni ya hapo Marsabit, mahali panaitwa Saku. Hapo maduka zinavunjwa sana, lakini yale mambo ya watu kuuana kama vile zamani yameisha na tunashukuru Mwenyezi Mungu."
}