GET /api/v0.1/hansard/entries/1291845/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1291845,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291845/?format=api",
"text_counter": 488,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Chute",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13583,
"legal_name": "Chute Mohamed Said",
"slug": "chute-mohamed-said"
},
"content": "Uliza mtu ametoka Turkana na Marsabit mambo ya usalama. Kuna watu wanasema wakora hawajulikani kule wametoka. Hakuna mkora hajazaliwa na hana baba wala mama. Wanajulikana hata zile vijiji wanakotoka. Kwa hivyo, hakuna mtu anaweza kuja kuua watu na isemekane yeye ni mkora. Hakuna kitu kama hiyo. Wale wakora tunajua ni wale wako Nairobi ambao hunyang’anya watu vitu vyao. Kwetu nyumbani, tunajua mkora ametoka wapi, baba na mama yake ni akina nani, hata ukoo na kabila tunazijua. Kwa hivyo, watu wasije mbele ya Bunge la Seneti kusema hawajui hao wakora ni akina nani. Tuambiane ukweli. Bw. Spika wa Muda, kama tunataka nchi ifaulu, shida iliyo Sondu sasa hivi inafaa itatuliwe kwa haraka kabisa, kwa sababu itaendelea na itafikia kama Marsabit ambapo watu mia tano wanakufa. Ninawaomba ndugu zetu Maseneta walio hapa, tafadhali, msiwe na hasira kwa roho zenyu mpaka kuingie shida ambayo watu wataenda kuuwana. Sisi ndio tunajua shida hii ya watu kukosana. Mvumilie. Ninaomba Serikali ichukue hatua kali kabisa kwa wale watu ambao leo wamewaua hao watu. Hii ni kwa sababu, wasipochukua hiyo hatua, wengine watakufa. Jukumu ya Serikali ni kuchunga maisha na mali ya wananchi wa Kenya. Hiyo iko katika Katiba. Kuna kitu kinaitwa blame game ama kulaumiana ---"
}