GET /api/v0.1/hansard/entries/1291849/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291849,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291849/?format=api",
    "text_counter": 492,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Asante sana, Mstahiki Spika wa Muda. Leo ni siku ya huzuni. Kama kuna siku ambayo tunafaa kuwa tumeungana tukijadili maneno ni leo. Kifo sio kitu cha kutaniana. Nimetoka Kirinyaga Kaunti ambapo nimezika watoto zaidi ya kumi na watano saa hii. Ni watoto ambao wamekuwa wakifanya kazi katika vyombo vya usalama kwa sababu ya michafuko. Hii ndio maana nasema kwamba huu ni kama mtego wa panya, unaingia waliokuwemo na wasiokuwemo. Kwa hivyo, tunapoongea mambo ya usalama Sondu, Turkana, Marsabit na kwingineko, ni vizuri tujue ya kwamba jambo hili tunahusika sote na linaweza kutupata. Pia juzi nimekuwa Turkana na jana nimekuwa Migori na Sen. Oketch Gicheru. Wakati tulikuwa Turkana tuliweza kutembea sehemu za Katilu Irrigation Scheme na tukaenda mpaka Ziwa Turkana. Katilu ni mahali ambapo kuna uwezo wa kuzalisha chakula ambacho kinaweza kulisha nchi nzima. Lakini hili haliwezekani kwa sababu ya shida ya usalama. Wawekezaji ambao wanaweza leta na kuwekeza katika mipango tofauti ya maendeleo hawawezi kufika mahali pale. Nalisikia watu wakiongeo mambo mengi lakini pia ningetaka niseme ya kwamba, wakati niliangalia Waturkana, pia mimi nilijawa na huzuni. Ukiangalia upande wa Sudan kuna Toposa, upande wa Uganda kuna Karamojong na upande wa Ethiopia wako na Oromo. Hata hivyo, wakati kunakuwa na mauwaji, tunakimbia sana kusema ni fulani wanauwa. Mimi sijawahi kuona watu walio na amani kama wale wakati tulienda pale. Hata hivyo, pia Mswahili anasema, ukiona manyoya ujuwe imeliwa. Haiwezekani ya kwamba usikie Marsabit, Turkana, Samburu na kwingeneko, wanalia. Lazima uangalie pia, kwani ni kiungo gani kinakosa. Hii ni kama chumvi inapatikana ndani ya chakula chote. Itaonyesha kwamba kuko na shida mahali ambapo mpaka tuangalie na tutatuwe kwa sababu shida zimekuwa mingi. Nilipokuwa mahali pale Katilu katika maeneo ambapo nilikuwa naambiwa ni mahali pa hatari, singesema kwa sababu tulikuwa na kikosi kubwa sana cha usalama. Hata hivyo, wakulima ambao wako kule hawana bunduki au usalama. Tunatarajia vipi wale watu kuzalisha mazao kama hawana usalama wa kutosha? Nikiongezea, mambo ya Sondu, kuna Serikali ambayo iko kwa mamlaka. Nimesikia kwamba hiyo mitafaruku ilianza kitambo wakati wa Mhe.Rais Moi. Kama wale wanafanyikazi kama vile vyombo vya usalama katika sehemu ile hawawezi kufanya kazi, wanafaa waondoke. Kama hatuwezi kumalizana na shida za Sondu, tutawezaje kumalizana na shida za wale wako na mabunduki kule Haiti? Ni vyema tugange ya kwetu kwanza kabla hatujaenda nje. Kwa hivyo, mimi ningehimiza kwamba tukijadili mambo kama haya, tushikane pamoja, tuonge tutatue kwa sababu hii Kenya yote ni yetu. Juzi nilipokuwa Migori tulienda na Sen. Oketch Gicheru katika migodi ya kuchimba madini. Hata hivyo, bado nilikuwa nasikia watu wengine wanaongea lugha ya"
}