GET /api/v0.1/hansard/entries/1291929/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291929,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291929/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika. Hili swala tunalojadili ni tatanishi kwa sababu ni mojawapo ya mbinu za kikoloni. Mbinu gandamizi na za kukanyagia wapiga kura husika nafasi ya kuwakilishwa katika Mabunge ya kaunti na ya kitaifa. Kamati ambayo utaipa majukumu haya ya kuchunguza na kuleta ripoti, itakusononesha sana. Hii ni kwa sababu kuna vyama vya kisiasa ambamo wanasiasa walikuwa wanapiga debe, wakiuza sera za mageuzi na uhusishaji wananchi, lakini wakati wa uteuzi, watu hawa walishangaa. Waswahili husema asiyeamini ya Musa, huyaona ya Firauni. Walioteuliwa kwa makaunti mbalimbali Kenya hii ni watalii wa kisiasa. Ni wafyonzaji wa nafasi za kisiasa. Ni watu ambao nitasema ni kupe wa kiasa. Wanafyonza jasho na jitihada za wapiga kura katika kaunti husika. Bw. Spika, viongozi hawa wa kisiasa ni kama mafarisayo, hata wengine wako hapa na wanatuahidi mabadiliko, lakini katika kaunti wanazotoka wananchi wanashangaa. kuna tume ya majadiliano ambayo inaendelea sasa na mimi ninaomba kwamba jambo hili lijadiliwe na tuweke sheria mapema."
}