GET /api/v0.1/hansard/entries/1291932/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291932,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291932/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "The Senate Majority Leader",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": "kupata chakula cha mchana, alizungumza na kusema hapa ndani kuna watu wabaya. Hawa watu wanafanya hivi na vile. Nimemsikiza tena akizungumza sasa. Amezungumza akasema kuna mafarisayo na kisha akasema wako hapa ndani. Nafikiri sio vizuri yeye kuruhusiwa kuelekezea kidole cha lawama watu ambao hawataji kwa majina. Kwa kweli ninajua mimi sio mmoja wao lakini kwa sababu ya hawa marafiki zangu, ndugu zangu Maseneta, ningependa kujua hawa ni akina nani. Kwa sababu akiwachiwa fursa hii ya kueleza na kuwalimbikizia lawama wenzake bila kusema ni akina nani haswa, nafikiri sio vizuri. Ni vyema awaeleze kwamba akisema hapa anamaanisha wapi. Ni hapa bungeni, Kenya, Barani Afrika ama dunia kote? Ni vizuri tuelewe. Asante, Bw. Spika."
}