GET /api/v0.1/hansard/entries/1291934/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1291934,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291934/?format=api",
"text_counter": 52,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Naomba hisani na msamaha kwa yeyote ambaye nimemdhuru kwa matamshi yangu. Ni jambo la kisiasa ambalo nadhani nitalijadili wakati mwafaka lakini kwa sasa naondoa sentensi hiyo. Nikimalizia ni kwamba, mjadala huu natarajia kwamba utachukua mwelekeo mwafaka ambao utawapa Wakenya katika pembe mbalimbali nafasi za kuwakilishwa na wenzao ambao wanawajua, wanawaelewa, wamepiga kampeni nao na wana mwelekeo mmoja wa kisiasa. Haya yote ni ili Kenya kisiasa na kidemokrasia iwe ni nchi ambayo unavuna kile ulichopanda na sio kwamba unatuzwa kwa uzembe ama kutuzwa kwa kuwa na falsafa ya fisi ambaye anatarajia kuvuna ama kupambana na mkono ambao hauanguki kihalali lakini kunyakua kwa lazima. Bw. Spika, naomba kwamba kutoka sasa kwenda mbele, vyama vya kisiasa vizingatie demokrasia na wale ambao Seneta wa wengi alisema, walemavu, wanawake na wazee, vile vile wapewe nafasi na vyama vya kisiasa na kuchaguliwa kama wakilishi wa Mabunge ya kaunti na kitaifa. Ukiangalia awamu tatu zilizopita, mfumo wa 2013 wanawake walikuwa wengi. Ukija mwaka wa 2017, kukakuwa na mchanganyiko na walemavu. Kwa sasa, pia kunatofauti. Lazima ieleweke vizuri. Wale ambao watateuliwa ni mfumo upi na wale ambao chama kinachagua wapewe nafasi sio tume ya uchaguzi kuamulia vyama vya kisiasa ni nani ambaye watamchagua."
}