GET /api/v0.1/hansard/entries/1291941/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1291941,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291941/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, asante kwa kunipa nafasi ili nitoe maoni yangu kwa ufupi kuhusu hii Ardhilhali ambayo iko mbele yetu. Bw. Spika, pengine shida iliyoko wakati huu ni kwamba sheria ya tume ya uchaguzi ya IEBC inasema kuwa wale watakaopewa nafasi za kuteuliwa katika jimbo gatuzi ama Bunge kuu, wanajiandikisha mapema kabla ya watu kupiga kura. Unapata wakati watu wanaenda kupiga kura, watu wazuri na wanasiasa ambao wamekomaa wanashindwa kwa bahati mbaya. Inakuwa hawawezi kuregeshwa kwa orodha ambayo iliandikwa na maafisa wa IEBC. Mtu wa siasa ambaye amejitolea kwa chama anakosa nafasi ilhali mwingine kwa sababu ya pesa ama kujuana na wakuu wa chama kile anapewa nafasi. Ardhilhali hii inafaa kuungwa mkono kwa njia zote. Itakapopelekwa kwa kamati husika, waambie waangalie ile sheria ya IEBC. Inafaa kubadilishwa na turudie ile sheria ya zamani. Tungojee uchaguzi umalizike ili tutafute watu wetu wa chama na ambao hawakufaulu wawepewe zile nafasi ili watusaidie. Pia wanafaa kuweka ghadhabu na faini kali kwa wakuu wa chama wanaochukua pesa na kuendeleza ufisadi. Wanabadilisha majina na kuweka ya wale wasio katika kaunti na kuwapitisha kuwa wawakilishi wadi kule nyumbani. Sitataja jina la kaunti lakini kuna kaunti jirani ya Tana River ambako Orange Democratic Movement (ODM) walileleta wawakilishi wadi kutoka nje. Watu walikasirika katika kaunti ya Kilifi na hawakutaka kuwaapisha wale watu. Ikawa ni shida. Lazima tuiangalie hii ardhihali na kuiunga mkono. Tunataka watu kutoka nyumbani wapewe nafasi hizi. Kwa hayo mengi, lazima tuiangalie sheria na tuiunge mkono hii ardhilhali kabisa, ili haki ifanyike kwa wanasiasa wanaotoka kwa magatuzi yetu."
}