GET /api/v0.1/hansard/entries/1291954/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291954,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291954/?format=api",
    "text_counter": 72,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika. Ningependa kuunga mkono Ardhilhali hii ambayo iko mbele ya Bunge la Seneti. Tumekuwa tukitumia nafasi ya wale wanaopendelewa na vyama vyao kuteuliwa vibaya. La kwanza, inajulikana bayana kuwa wanaochaguliwa huwa ni wapenzi na marafiki wa wale wanaowateua. Ambao huwa ni viongozi wa vile vyama ambazo zinafaa kuteua. Wateuliwa wa kupendelewa wanafuata ule mkondo wa ule aliyewateua. Mara nyingi tunajipata kwenye njia panda kwa sababu ya wale ambao wanateuliwa. Ardhihali hii ni kuhusu wanaoteuliwa kwenye mabunge ya kaunti zilizoko mashinani. Uteuzi kwenye kaunti ama hapa Bungeni umetumika vibaya. Ndugu yangu Sen. Mungatana ametaja kuwa Kaunti ya Kilifi ilikuwa mojawapo ya wale waliolalamika, sijui aliambiwa na nani na alijuaje. Sikuweza kupinga hilo kwa sababu ilikuwa ni kweli. Wakati huu, 2022, mambo ya kuteuwa namna hiyo yalikoma. Hii ni kwa sababu tuliweza kurekebisha na wale walioteuliwa ni wakaaji na watu wa chama cha ndani ya Orange Democratic Movement (ODM) Bw. Spika, vile vile, ikiwa itawezekana, Kamati ambayo itachunguza hii, iweze kuja na recommendation ama kusahihisha kabisa ya kwamba sheria mwafaka inaweza kutengenezwa ili kuona ya kwamba mambo haya ya watu kupendelea jamaa zao yatafika mwisho. Ukiwa utateuliwa, basi uteuliwe ikiwa wewe ni mkaaji wa ile kaunti ambayo unatoka ama sehemu ile ambayo wewe unafanyia kazi ama unajihusisha na chama katika ile kaunti ambayo utataka kuteuliwa. Sio kutoka katika Kaunti moja uende nyingine kunyanyasa wale watu wanaoketi katika ile kaunti yao. Kwa hivyo, tabia kama hii ikome. Tuone ya kwamba watu wote walio kwenye vyama vyao watatendewa haki kulingana na uteuzi wa wale wanaopendelewa na vyama vyao."
}