GET /api/v0.1/hansard/entries/1292057/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1292057,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1292057/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "ambao wanashawishi wakenya kufanya ushoga. Kamati hii yafaa ifanye kazi nzuri kwa sababu swala la ushoga ni la kipepo. Korti zetu hazijasaidia kutatua hili swala kwani wamepitisha rulings ambazo zinasema kuwa ni haki ya mashoga na wasagaji kuwa na vyama vya ushirika. Ya pili ni Kauli ambayo imetolewa na Sen. (Dr.) Khalwale, kuhusu viwanja vitakavyo tumiwa wakati wa Africa Cup of Nations(AFCON), 2027. Lazima kuwe na uwazi wa mbinu na vigezo ambazo zitatumika kuangalia viwanja vitakavyo tumika, kama kuna manufaa yoyote kama vile sports tourism, wakenya wote wafaidike. Nimeona kwenye vyombo vya habari kuwa kuna kiwanja kitakachojengwa kitakachokuwa na uwezo wa kuwa na viti 60,000. Kiwanja kitajengwa wapi? Nikisikia masuala ya viwanja mimi hucheka kwa kuwa serikali ya Jubilee wakati walikuwa wakiuza sera walisema kutakuwa na viwanja vya kimataifa katika kila Kaunti, lakini hii ilikuwa mbinu ya kupata kura. Kufikia leo Kaunti ya Taita Taveta haina uwanja wa kitaifa wala wa kimataifa. Kauli iliyosomwa kuhusu mavuno ama post harvest prices – ni jambo la kuhuzunisha kwamba tumekuwa na njaa, shida ya mfumuko wa bei na hivi sasa wakulima wamepata mazao lakini wanauza mazao haya kwa bei ya hasara. Ni jambo la kuudhi kama serikali haiwezi kujiandaa. Walisema kuwa wataenda Zambia kulima mahindi na kuleta Kenya kukabiliana na mfumuko wa bei. Hivi sasa wakulima wamevuna na hakuna mbinu wala mpangilio wa kununua chakula kutoka kwa wakulima. Serikali yetu lazima ijizatiti ili waweze kulisha wananchi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}