GET /api/v0.1/hansard/entries/129354/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 129354,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/129354/?format=api",
"text_counter": 296,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Haji",
"speaker_title": "The Minister of State for Defence",
"speaker": {
"id": 26,
"legal_name": "Yusuf Mohammed Haji",
"slug": "yusuf-haji"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, kazi ya mkulima ni kwenda kulima shamba lake. Mchungaji pia anaenda kuchunga ngâombe na ngamia wake. Sisi tumechaguliwa kuja hapa kutengeneza sheria na pia kupata nafasi ya kuweza kuungana na watu wetu, kukaa pamoja nao, kujua shida zao na kuwasaidia katika matatizo yale ambayo wananchi waliotuleta wamechungulia. Hatukuja hapa kukaa Nairobi kula raha na maji mazuri; kutembea kwa barabara nzuri au kwenda hospitali"
}