GET /api/v0.1/hansard/entries/129356/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 129356,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/129356/?format=api",
    "text_counter": 298,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "nzuri peke yake. Hiyo siyo kazi ambayo tumechaguliwa kuja kufanya. Isitoshe, ninaona ya kwamba Bunge leo linataka kuwa mshtaki na pia mahakama ya kuhukumu hiyo kesi. Kama kuna chochote ambacho kimeenda kombo, tuseme kama uteuzi wa Bw. Ringera kwa mara ya pili yamekuwa makosa, nafikiri kuna nafasi ya wale ambao wanafikiria kuna makosa yamefanyika kuchukua hatua inayofaa kisheria kuliko kuchukua Bunge mateka kwa sababu ninaona ya kwamba Bunge linachukuliwa mateka kwa sababu ya jambo linalohusu mtu mmoja. Kwa hivyo, ninataka kuomba ndugu zangu hapa ya kwamba ni vizuri tuangalie maslahi ya wananchi wengi wa Kenya. Leo watu wanakufa kwa sababu ya njaa; sio kwa makosa ya binadamu lakini kwa Mwenyezi Mungu anatupa adabu kwa kukosa njia ambayo inafaa kwa viongozi kufanya katika kutekeleza wajibu wao kwa wale ambao wamewachagua. Nafikiri tukitoka hapa tuende sehemu za uwakilishi Bungeni na tufanye mipango ya kuomba mvua, Mwenyezi Mungu ataona kwamba hata viongozi wako na wananchi wanaomba Mungu na kwa hivyo mvua huenda ikaja na watu wakatoka kwa taabu."
}