GET /api/v0.1/hansard/entries/1294267/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294267,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294267/?format=api",
"text_counter": 71,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa nafasi ili nitoe maoni yangu kuhusu sheria hii ya Digital Health Bill ambayo tunaileta mbele ya Seneti. Leo niko na furaha sana kuwa kati ya wale wabunge wa Seneti ambao tunajihusisha kujenga hii Kenya ambayo itakuwa baadaye, Kenya mpya ambayo watoto wetu na vitukuu wetu wataishi ambapo sisi hatuishi saa hii. Nilikuwa naangalia runinga na nikaona gari ndogo ambalo lilikuwa linabeba watu wawili. Hilo gari ndogo walikuwa wanaliita katika runinga hiyo ama documentary, e- Shuttle. Hili ni gari ambalo huko mbele wamepanga ya kwamba, ukipiga simu, hilo gari litajua pahali uko na hilo gari linaonyesha uso wako. Hilo gari halina dereva, ni zaidi ya Uber na linatumia umeme. Bw. Spika, nchi ambazo zimeendelea zinatengeza data na taarifa. Sheria hii ambayo tunataka kupitisha inataka kuigeuza nchi hii ili iende mbele kwa mambo ya kuweka taarifa zetu kwenye tarakilishi kidijitali. Tunafaa kutengeneza sheria hii na tuipitishe kwa haraka sana. Watu wanapoenda hospitali kila mmoja anabeba kijikaratasi au kitabu ili amuone daktari. Daktari anaiandika ili mgonjwa yule apate matibabu. Akirudi siku nyingine kama kitabu kimepotea, basi daktari anauliza maswali mapya kwa sababu hakuna kumbukumbu ya taarifa yake. Ukipata ajali au mama akienda kujifungua, rekodi yake ya afya haijulikani. Pengine amepelekwa mahali pana matibabu ya juu zaidi kama Hospitali ya Rufaa. Akifika kule historia yake ya afya haijulikani kwa sababu ni kitabu kinachotumika na ni rahisi kukipoteza. Sheria hii itatupeleka mbele kwa mambo ya afya nchini. Miaka itakuja, itaenda na itaisha. Wakati tutakapo staafu mjini kwetu Ngao London, Mwatate katika Kaunti ya Taita-Taveta tutapata magonjwa kwa sababu ya uzee. Ukienda katika Hospitali ya Umma na rekodi zako zote ulipokuwa unaishi na kuenda ziko, basi yule daktari atakupa utambuzi na dawa zinazofaa na utatibiwa vizuri kulingana na shida uliyonayo. Hayo hayatatekelezwa kwangu au kwa wakubwa na wazee wanaostaafu pamoja na wafanyi biashara pekee, itakuwa kwa kila mwananchi wa Kenya. Bw. Spika, sheria hii ikipitishwa leo, itaenda kubadilisha kabisa hali ya Kenya kuhusu mambo ya afya. Naomba wenzangu na wote watakao angalia sheria hii, waiangazie na waipitishe kwa sababu itatusaidia sisi na watoto wetu pamoja na kila mtu humu nchini. Hii itakuwa safari ndefu kwa sababu rekodi hizi za afya ni za ma milioni ya wakenya na zitakuchukua muda mrefu kuziweka sawa sawa. Tukiipitisha sheria hii leo, miaka 10 au tano kuendelea mbele tutakua tumechukua hatua kubwa sana. Naomba wenzangu tushirikiane na tuipitishe katika Seneti hii kwa uharaka sana. Vile vile, wakati serikali ya kaunti inaelekea kufanya---"
}