GET /api/v0.1/hansard/entries/1294278/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294278,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294278/?format=api",
"text_counter": 82,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa nafasi hii ili nichangie kuhakikisha kuwa mfumo wa kidijitali wa afya unaafikia malengo ya wakenya. Kwa muda mchache ambao nimepitia Mswada huu, nimeona kuwa Mswada huu utahakikisha kuwa mfumo huu una uwezo wa kuhusisha zahanati au hospitali nchini ili zitambulike. Vile vile, wauguzi katika sekta mbali mbali watawajibika kwa sababu taarifa yao itakuwa katika mfumo huu. Itahakikisha kuwa madawa yanaoyotoka katika viwanda husika na kupekela katika hospitali pamoja na wanazozitumia watanaswa katika mfumo huu."
}