GET /api/v0.1/hansard/entries/1294280/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294280,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294280/?format=api",
"text_counter": 84,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Madawa mbali mbali yataafikiwa ama kupatikana kutokana na mfumo huu. Utahakikisha kuwa ujumbe wa kibinafsi na arafa za kidaktari pamoja na mapendekezo ya madawa yatawekwa vizuri dhidi ya wale wanaonyemelea magonjwa au maarifa ya watu binafsi kwa minajili ya kupata wanachotaka. Mengine ambayo yanaafikiwa katika mfumo huu ni kuwa yote yatafanywa kidijitali na kupitia mfumo wa kiteknologia ili kuhakikisha kuwa nyenzo au taasisi za kifedha zinazo shiriki kuhakikisha mfumo huu zitaafikia malengo ya serikali. Wakati pesa zitakapo lipwa kwa watu hususan, watanaswa katika mfumo huu ili pasiwe na mambo kama ilivyokuwa ada; watu kutozwa malipo ya juu kinyume cha sheria ama taasisi za kifedha kupata mapato kinyume na matarijio ya wagonjwa na serikali. Naunga mkono Mswada huu kuhakikihsa kuwa Kenya inasonga mbele. Ningependa kuongeza kuwa nimeyaona mapendekezo hapa kuwa Waziri husika atakuwa anapeana mwelekeo jinsi ya kuitumia data itakayopatikana kutoka kwa wakenya ili kuafikia au kufanya mazuri katika nchi ya kenya. Ningependa iwekwe katika misingi mathubuti, kwamba data hii ni ya wagonjwa ama wahusika wa sekta ya afya na itabaki kuwa hivyo. Isije ikatumika vingine pasipo idhini ya mgonjwa ama mhusika. Jinsi tunavyo elewa Kenya hii, japo wanasema itasaidia katika utafiti na data, inafaa watuambie ni utafiti upi. Kama ni utafiti wa kuleta madawa ya kukimu mahitaji ya wakenya ni sawa, lakini si kutumiwa kujulikana kuwa mheshimiwa fulani ama mtu fulani, iwapo ni mgonjwa ukitaka kumfinya unatumia mbinu hii. Hili jambo hatutakubali. Naomba tutakapounda sera, iweze kuzingira na kuweka data ya wakenya vizuri ili tusije tukajuta siku zijazo. Kwa mafupi hayo, naungo mkono Msada huu."
}