GET /api/v0.1/hansard/entries/1294332/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1294332,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294332/?format=api",
    "text_counter": 136,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bw. Spika. Ninaunga mkono Mswada huu wa mambo ya afya. Hii ni kwa sababu afya ni kila kitu ulimwenguni. Tukipitisha Mswada huu, tutafanya vizuri kwa sababu Serikali ya Kenya Kwanza iko na maono. Nchi za ngambo kama vile Marekani, Turkey, Dubai na zinginezo zilishapitisha mambo haya. Kwa hivyo, sisi pia tuko katika mstari wa kuyakupitisha. Tunapofanya mambo haya, tunafaa tuangalie wafanyikazi ambao waliajiriwa wakiwa na miaka 20 na sasa wako na miaka 60. Mswada huu utatusaidia. Hii ni kwa sababu, kwa mfano, mtoto akizaliwa, rekodi yake yote itakuwa kwa mitambo ya kidijitali. Swali langu ni ikiwa mtu atasitafu atafaidika vipi? Nchi za ng’ambo, mtu akifika miaka sitini huwa anaangaliwa na Serikali. Gharama yote ya maisha yake akiwa amestaafu huwa ni juu ya Serikali. Ningeomba, hata kama tunapitisha, tuweze kuangalia wale wafanyikazi na akina mama wazee. Pia sisi tukizeeka, itatusaidia na njia gani? Upande wangu wa Kaunti ya Embu tunaunga mkono mambo ya hayo ya machine."
}