GET /api/v0.1/hansard/entries/1294376/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1294376,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294376/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Bw. Spika, nilinde kutokana na watu wenye--- Mswada huu utasaida sana kuhifadhi data za wagonjwa. Jambo la pili, kuna kaunti ambazo hazina wauguzi na wataalamu wa kutosha. Utapata kwamba kaunti zenyewe ni kubwa pia. Hapo kuna uwezekano wa kuwa na daktari mtaalamu mmoja katika eneo moja. Mgonjwa anapohudumiwa katika zahanati ambazo ziko katika wadi, yule mtaalam mmoja anaweza husishwa. Ikiwa mtu amevunjika mguu, atapigwa picha ambayo itatumwa kutafsiriwa, kisha ripoti kurudishwa na mgonjwa apate matibabu. Itapunguza msongamano katika hospitali zetu. Sasa hivi, ripoti zetu za afya huandikwa kwa karatasi na daftari."
}