GET /api/v0.1/hansard/entries/1294402/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294402,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294402/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili nuinge mkono Mswada huu ambao unazungumzia kuwekwa kwa data katika mfumo wa kidijitali. Nampongeza aliyekuja na fikra kama hii. Mimi ni Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Information, Communication and Technology (ICT). Tukiwa katika vikao vya Seneti Mashinani kule Kaunti ya Turkana, tuliweza kuizuru hospitali moja na tukapata kuonyeshwa jinsi data inahifadhiwa na huduma kupeanwa. Watu wa Lodwar wako mbele zaidi kuliko gatuzi zingine kama yangu, Kaunti ya Mombasa, 001. Pale picha za wagonjwa zinapigwa na zinayotumwa kwa daktari ambaye anasoma taarifa yake na inapunguza ile safari ya kupeleka na kurejesha. Picha inatandazwa kutumia vyombo vya kidijitali na huduma inapatikana. Naipongeza Kamati ya afya katika Bunge la Seneti kwa kuleta wazo hili ambalo litawasaidia akina mama wajawazito wanaohitaji huduma mara kwa mara. Mara nyingi akina mama kama hawa wanapoenda hospitalini katika maeneo mengine huwa wanapata shida kwa sababu wanaanza ule mchakato mpya. Hivi sasa, data yao itakuwa ina hifadhiwa kidijitali. Itakuwa rahisi kwa daktari atakaye tembelewa kupata taarifa ya mama kama yule bila kuanza upya. Kwa hayo, mengi au machache, naomba kuunga mkono Mswada huu. Asante."
}