GET /api/v0.1/hansard/entries/1294404/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1294404,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294404/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, najiunga na wenzangu pia kuunga mkono Mswada huu wakuweka stakabadhi za afya katika njia ya kidijitali. Sheria hii imechelewa sana katika nchi hii. Tayari madaktari kwenye hospitali nyingi wanafanya vile bila ya kuwa na hii sheria. Madaktari wengi wanaofanya kazi ya kupiga picha kwenye radiolojia, wanayo nafasi ya kusoma ripoti kwa mfumo huu. Pia wanaweza kuandikia daktari riporti akiwa pengine Kaunti ya Kisumu na yeye akiwa katika Kaunti ya Meru. Sheria hii imechelewa sana kwa sababu mambo ambayo yanazungumziwa tayari yanatumika na madaktari na wahudumu wengine wa afya. Pia sheria hii itasaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali zetu. Baada ya daktari kupata ripoti, mgonjwa hana sababu ya kurudi hospitalini. Daktari anaweza kumpa maagizo ya dawa anazohitaji kununua kutoka duka la dawa. Mswada huu una mambo mengi mazuri na singependa kuongeza zaidi ya hapo. Hii sheria imekawia kwa muda mrefu wakati sisi kama taifa tuliihitaji. Asante."
}