GET /api/v0.1/hansard/entries/1294408/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294408,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294408/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "hali ya mgonjwa huyu. Taarifa ya mgonjwa inaweza kusomwa na daktari mkuu au mzoefu wa kazi aliye Kaunti ya Nairobi na kumsaidia mgonjwa yule bila ya kusafiri. Huu Mswada utasaidia kuinua uchumi wetu. Watu wengi hawana hela na wanatarajia kuchangiwa na watu ili wasafiri kutoka sehemu mashinani hadi mjini ili wapate matibabu. Mswada huu utasaidia kuwapatia wagonjwa afueni. Wakati stakabadhi za mgojwa zimehifadhiwa vizuri daktari atapata historia ya mgojwa wake. Historia inahifadhiwa vizuri katika ufuo huo. Daktari wa kwanza, pili na wa tatu watafuatilia bila kukosea utambulizi wa mgonjwa. Tukiwa na stakabadhi zilizohifadhiwa kidijitali, Serikali itapata ujuzi wa magonjwa ambayo yanadhiri sehemu tofauti. Ninaunga mkono Mswada huu ambao umechelewa. Ungekuwa umepita awali ili Wakenya wapate afueni kiuchumi na hata maradhi yao yashugulikiwe na madaktari hata wakiwa nchi za ng’ambo. Nashukuru na kuunga mkono."
}