GET /api/v0.1/hansard/entries/1294531/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1294531,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294531/?format=api",
    "text_counter": 335,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bi. Spika wa Muda, jambo la kwanza, ninaunga mkono kipengele hicho cha kuambia watu wa National Health Insurance Fund (NHIF) waombe kazi mara ya pili. Kama wako qualified, waombe kazi. Imeandikwa kama hawatapata hizo nafasi, wako na nafasi ya kuomba retirement ama wapelekwe kwa nafasi zingine za Serikali. Muhimu ni, saa hii, NHIF vile ilivyo, imetudhulumu sana sisi watu wa kutoka kaunti ya kando. Kwa Kaunti kama Tana River, utakuta watu ni wachache sana ambao wameandikwa kwa NHIF. Kwa hivyo, wacha hii NHIF ivunjwe na hii mamlaka mpya iandike watu kutoka kaunti zote. Hivi ilivyo, ni kama NHIF ni jopo la watu wa Kaunti ya Nairobi pekee yake. Kwa hivyo, wacha hii ivunjwe, watu waandikwe wakitoka kaunti zote kwa sababu hii ni bima ya watu wote wa kaunti zote. Tunaomba ivunjwe, haswa NHIF, tupate nafasi na sisi watu wa kutoka Kaunti ya Tana River tuandikwe. Pili, imesemekana hapa kwamba hii mamlaka mpya ambayo inatengenezwa itakuwa na nafasi ya kuandikisha watu wapya kutoka sehemu mbalimbali watoe hizo huduma za afya. Tunataka watu wakienda kutafuta watu wakija Kaunti ya Tana River, waangalie wale ambao tayari wanasaidia watu. Pale chini, kuna watu ambao wanasaidia watu sana."
}