GET /api/v0.1/hansard/entries/1294533/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294533,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294533/?format=api",
"text_counter": 337,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "madaktari wa kawaida na Chief Clinical Officers wamefungua vituo vyao vidogo lakini unapata NHIF hawawaandikishi. Inakuwa kwamba vituo vikubwa kutoka Kaunti ya Nairobi ndio vinapeleka branches Kaunti ya Tana River na zinanyima watu wa afya kutoa nafasi kwa wafanyibiashara ambao wako na nafasi ya kusaidia watu wetu. Ninaunga mkono wapewe nafasi ya kuandikisha watu wapya ambao watatoa huduma za afya. Waangalie wale ambao tayari wanasaidia wananchi huko chini. Mwisho, nilikuwa naomba kipengele kimoja kiingizwe. Ya kwamba wafanyikazi wa Serikali, baada ya kupitisha hii na ile sheria ya digital, Wabunge, Maseneta na wakubwa wa Serikali wasipewe nafasi ya kuenda kwa private hospitals. Sote tuwe tunaenda kwa public hospitals. Tukifanya hivyo, hizi pesa ambazo tunatoa sasa kwa hii mamlaka mpya zitatumika vizuri. Tunataka watu waanze kusema ukweli sio kudanganya"
}