GET /api/v0.1/hansard/entries/1294690/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1294690,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294690/?format=api",
    "text_counter": 56,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mundingi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "umefanya. Tukiendelea hivyo, Serikali yetu ya Kenya Kwanza, kwa hiki kipindi cha miaka mitano, itaeendelea vizuri. Hata wale watu ambao wanaendesha magari kwa barabara saa hii, sisi wenyewe tunafurahia na pia wezi wanakuogopa. Pia watu wale ambao walikuwa wanarusha mawe wanakuongopa kwa sababu ulisema ya kwamba hakutawahi kuwa na maandamano tena na sasa tunaendelea vizuri. Swali langu ni kuhusu Turkana. Tulipotembea huko wakati wa Seneti Mashinani na kwa kipindi cha miaka mingi kule ni mambo ya vita tu. Sasa hiyo ndiyo njia na hata wale viongozi wanajificha pale. Kaunti ya Turkana, kwa kipindi cha miaka kumi wamepewa billioni mia moja na thelathini na kaunti zingine kama Embu imepata bilioni sita kwa hivyo ni bilioni kama hamsini kwa miaka kumi. Hata hivyo, tulipoenda pale, hakukuwa na pesa iliyokuwa inaonekana lakini wanajificha kwa mambo ya Security . Kwa uwerevu wako ninakuomba, pale sio nguvu itatumika, unaweza tumia huo uwerevu wako ambao unataka kutumia Kenya ndipo tuweze kuokoa watu wa Kaunti ya Turkana. Tunakuomba ikiwa inawezekana, utumie makanisa na viongozi uone kama inaweza kuokoa Kaunti ya Turkana. Asante."
}