GET /api/v0.1/hansard/entries/1294742/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1294742,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1294742/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika wa Muda kwa kunipa hii nafasi. Kwanza, ninamshukuru Waziri kwa kazi nzuri anayofanya katika Idara ya Usalama. Unahitaji moyo, tajriba na weledi kukabili vishindo vya usalama nchini. Katika majukumu ya kulinda usalama katika sehemu tofauti tofauti, mara nyingi maafisa wa polisi hutumwa katika eneo fulani. Kwa yamkini mwaka mmoja, Kirinyaga tumezika takriban watu nane walio chini ya umri wa miaka 27. Ningependa kuuliza Waziri; je, kuna uwezekano maafisa wanaotumwa ni makurutu, ambao hawana uzoefu wa kutosha kwa mazingira wanayopata na ndio maana wanapoteza maisha? Wanapopoteza maisha, je, fidia yoyote inalipwa? Na je, fidia inayolipwa ni ya kutosha familia zilizoathirika? Ninauliza hivi kwa sababu familia nyingi zilizo na watoto katika Idara ya Polisi, wengi hutarajia kusaidika kutoka kwa hiyo kazi ambayo watoto wao wanafanya. Halafu zipo sehemu zenye vita kama vile Turkana na kwingineko ambako jamii tofauti zinazozana hasa kwa mipaka. Kuna uwezekano wa kuwekwa buffer zone ? Ninazungumzia sehemu ambayo polisi watakata labda kwa kulima ili wakinge mapigano baina ya jamii mbili. Kukiwa na buffer zone katikati, hata kama itatumika kwa kilimo, niko na uhakika kwamba mashambulio yatapungua. Asante, Bw. Spika wa Muda."
}