GET /api/v0.1/hansard/entries/129556/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 129556,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/129556/?format=api",
"text_counter": 498,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo tunaomba yajadiliwe na tukikaa hapa, Hoja ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Fedha ambayo hatujaikamilisha itakuwa imeiva kesho na tutaihudumia kama vile ilivyo. Tungependa kwenda tukijua kwamba wale ambao wametupatia majukumu ya kuja kuwaakilisha hapa, tumewasilisha yale walio nayo kikamilifu. Watatuuliza maswali magumu na moja yao ni hiyo Hoja ya Naibu Waziri na Waziri wa Fedha. Ya pili ni shughuli ya Msitu wa Mau. Umesikia wenzetu wakizungumza kwa undani. Jambo la kukata Msitu wa Mau umesababisha ukaukaji wa maji kila mahali. Hata kwangu kule Taita kumekauka. Sasa mnataka twende nyumbani kabla hatujamaliza hayo mambo? Ni nini tunakimbilia? Kwani mna watoto wa kunyonyesha? Hamna! Kama wapo muwalete tuwaone. Mheshimiwa mwenzetu amesema hapa kwamba hisia zake kwa mumewe amezibana ili ashughulikie mambo ya Bunge, nasi tunamuunga mkono. Lakini ni nini hiki hatuelezwi wazi wazi? Tumeuliza hapa; Bw. Ringera amepewa kazi lakini swala sio yeye bali ni njia ambayo imetumiwa kumpa kazi. Wengine wetu hatumfahamu wala hatumjui Bw. Ringera. Tunaona kazi yake. Wengine wanaiheshimu na wengine wanaipuuza. Lakini swala muhimu ni kuwa, kama wale Wakurugenzi wengine walipewa wadhifa wa kuhudumia taifa hili walifuata sheria na mkondo ambao umewekwa na sheria, kwani huyu Ringera ana nini? Kwa nini aletwe kinyumenyume? Kwa nini sheria isifuatwe hadi apewe kazi? Bw. Spika, jioni hii ninashangaa kusikia wenzetu wakisema kwamba wanaunga mkono Hoja ya kwenda nyumba ilhali hatujakamilisha maswala muhimu. Kwenda nyumbani haimaanishi kuwa unaenda kuhudumia watu wako. Kuna wengine hapa tutapewa likizo ya kwenda nyumbani lakini hawaendi. Watakuwa wanajibana hapa hapa mjini na tunawajua. Naomba niweke tamati."
}