GET /api/v0.1/hansard/entries/129681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 129681,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/129681/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Dr. Gesami",
    "speaker_title": "The Assistant Minister for Public Health and Sanitation",
    "speaker": {
        "id": 19,
        "legal_name": "James Ondicho Gesami",
        "slug": "james-gesami"
    },
    "content": " Bw. Spika, ninaomba kujibu. (a) Sina habari yoyote kuhusu mkurupuko wa ugonjwa wa tando za uti wa mgongo (yaani Meningitis) Wilayani Samburu, wala vifo vyovyote kwa muda wa wiki tatu zilizopita. Bw. Spika ninaomba ibainike ya kwamba kuna aina kadha za ugonjwa wa tando za uti wa mgongo kama vile meningococcal meningitis na cryptococal meningitis . Kwa sasa, ninazo habari kuhusu wagonjwa watatu ambao wamelazwa katika hospitali kuu ya Wilya ya Samburu wanaougua uvumbe wa tando za uti wa mgongo yaani cryptococalmeningitis . Wataalamu wamedhitisha kwamba wanao ugua ugonjwa huo huwa na viini ambazo hudhibitisha ukosefu wa kinga mwilini. Imebainishwa kwamba hali yao ya kinga mwilini imezoreteka sana. Kati ya hao watu, wawili ni wanaume na mmoja ni mwanamke."
}