GET /api/v0.1/hansard/entries/129682/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 129682,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/129682/?format=api",
"text_counter": 70,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Gesami",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Public Health and Sanitation",
"speaker": {
"id": 19,
"legal_name": "James Ondicho Gesami",
"slug": "james-gesami"
},
"content": "Naomba pia kufahamisha Bunge hili kwamba ninazo habari kuhusu kifo cha mvulana mwenye umri wa miaka 15 ambaye alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa malaria ya ubongo, yaani cerebral malaria . Kulingana na matokeo ya utaalam wa maabara, ilibaini kwamba ni malaria ya ubongo. Dalili zake hufanana na zile za ugonjwa wa uvimbe wa tando za uti wa mgongo yaani meningococcal meningitis. (b) Ugonjwa wa uvimbe wa tando za uti wa mgongo ni mojawapo ya maradhi 18 sugu, ambayo Wizara ya Afya ya Uma na Usafi, imeorodhesha kwa ukachero mwafaka sana. Taarifa zake hutolewa kila wiki ili kuthibitisha mikakati maalum katika kuangalia haya magonjwa 18."
}