GET /api/v0.1/hansard/entries/1299532/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1299532,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299532/?format=api",
"text_counter": 353,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Nasimama kama kiongozi aliyetoka ule mkoa ulioadhirika zaidi na wizi wa mashamba. Nasimama kwa uchungu kwa sababu imekuwa ni tabia. Naunga pia Sen. Orwoba kwa sababu kuna watu mahali wamekaa na wamejipanga ni jinsi gani watakuwa wakiibia Wakenya walalahoi pesa zao kwa kuwauzia mashamba ambayo sio yao. Ni jambo la kusikitisha sana kuona viongozi wakilumbana katika Taifa la Kenya wakati kuna wananchi ambao wako nje na hawajui watalala wapi. Mimi kama mzazi na kutokana na maswala yale ya El nino yamekuwa yakizungumziwa, naona ni bora, hawa waliotolewa katika haya majumba, kupelekwa zile nyumba ambazo wale wametuhumiwa, waliotajwa na DCI leo. Bi. Spika wa Muda, sisi kama Taifa ni wakati tuchukue mkondo mpya kama Serikali mpya katika Taifa hili. Chini ya Serikali ya Rais William Samoei Ruto tulizungumza maswala ya ardhi yatakuwa maswala ya serikali zilizopita na sio Serikali hii. Tukaongea kutakuwa na mazungumzo na watu kufidiwa. Mimi kama kiongozi, ningependa Bunge hili litenge sheria ya kuona yule atakayepatikana ameuzia mwingine shamba ambalo sio lake, apewe adhabu kali. Pia ningependa sisi kama Maseneta na viongozi katika taifa hili, tukubaliane ya kwamba ni uchungu kuona kuna watu katika ofisi za Serikali ambao walipiga mihuri ya kuwezesha wale wananchi kujenga maeneo kama yale. Ningependa kando na wale ambao waliwauzia hata wale ambao wako katika ofisi za Serikali hadi sasa, wachukuliwe hatua kali. Wale wote ambao waliwai kufanya kazi katika ofisi za Serikali za Ardhi, wafikiwe kwa sababu kuondoka katika ofisi ya Serikali haimaanishi mkono wa Serikali hautakufata pale ulipo. Wale waliwatendea dhuluma wananchi wa Taifa la Kenya kwa kusahihisha na kuweka sawa wizi wa ardhi ulioendelea pale Mavoko wafatwe na mkono wa sheria uchukue njia yake. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}