GET /api/v0.1/hansard/entries/1299714/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1299714,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299714/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa nafasi hii. Kwanza naanza kwa kuzungumzia Hoja ama jibu ambalo tunatafuta kuhusiana na kufutwa kazi kwa walimu ambao walikuwa wanaomba uhamisho kwenda katika maeneo ambayo yana usalama na ambayo kazi yao itashughulikiwa na Serikali. Ni kinyume cha matarajio kwa sababu Tume ya Kuajiri Walimu huandika waalimu kazi. Lakini, haiandiki maasifa wa polisi ama vikosi vya vigilante kazi ya kudhibiti usalama katika maeneo hayo. Sisi kama Seneti, lazima tusimame na waalimu. Iwapo mazingira ya kazi si mwafaka kuhakikisha wanatimiza majuku waliyopewa, lazima tuhakikishe kwamba wamepata yale wanayotarajia. Naomba Jumba la Seneti liamrishe TSC kuwarejesha kazini waalimu hao kwa sababu hawakupewa nafasi ya kujitetea. Pia ni kinaya kwa sababu, katika Jumba la Seneti na Serikali ya Kenya ambamo mimi ni mshiriki mkubwa wa Kenya Kwanza, viongozi wa maeneo haya walitazama kwa macho walimu walipokuwa wanafutwa kazi pasipo kupaza sauti. Sasa lazima tuwape haki walimu hawa ili wanafunzi wa nchi ya Kenya wapate yale ambayo wanastahili. Jambo la pili ni ile Hoja ambayo Mheshimiwa ametaja kuhusiana na gharama ya afya, ama zile pesa ambazo Serikali inapaswa kupata kwa mfumo wa National Health Insurance Fund (NHIF). Tukiangaza katika kaunti mbalimbali, tunagundua kwamba kaunti zimeanza kupata mpenyezi ama nyenzo za kupora pesa, kwa kuwapa watu binafsi ama wanabiashara kazi ya kulipa gharama za afya ilhali---"
}