GET /api/v0.1/hansard/entries/1299728/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1299728,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299728/?format=api",
    "text_counter": 190,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu Spika. Ninashukuru kwa sababu leo kauli nyingi zimesomwa na wenyekiti wa Kamati nyingi walikuwa hapa, akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu. Takriban Kauli tano zilizosomwa leo, zilikuwa kuhusu elimu. Ni maajabu kuwa na elimu bila walimu. Elimu haiwezi kuendelea vizuri katika nchi yeyote bila mwalimu. Mtoto anapozaliwa, anaanza kufunzwa na mwalimu baada ya miaka nane. Kama kuna mtu ambaye anafanya kazi nzuri, ni mwalimu awe wa shule ya msingi, sekondari na hata mwalimu yeyote yule. Kwa hivyo ninaomba kutoka leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu aende aangalie ni kwa nini kila wakati watu wanalalamika juu ya elimu. Utakuta mwalimu anafanya kazi lakini anapostaafu, halipwi pesa zake na hakuna marupurupu. Wakati mwingine, utakuta kwamba yeye ndiye anaenda kusahihisha mtihani. Ili tupunguze wizi"
}