GET /api/v0.1/hansard/entries/1299738/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1299738,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299738/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Nataka kuipongeza taarifa iliyoletwa na Sen. Munyi Mundigi na Sen. Cherarkey. Najua kuwa mfanyikazi yeyote wa serikali anapoajiriwa anapeana maelezo ya kuwa anaweza kufanya kazi mahali popote katika Jamuhuri ya Kenya. Kuna wakati ambapo maji yanazidi unga. Unapata sehemu zingine hazina usalama wowote na watu wanashambuliwa. Ni jukumu la Serikali kulinda mali na maisha ya mwananchi anapoenda sehemu ambayo maisha yake yako hatarani. Walimu walioenda sehemu ambazo hazina usalama walisema kuwa ni vizuri watolewe katika sehemu zile. Taasisi ya Elimu kuwafuta kazi ni unyama unaopaswa kukemewa na kila mtu. Walimu ni wananchi ya Kenya na wana uhuru na haki ya kufanya kazi popote wanapotaka. Kukiwa na hali hatari--- Tunaelezwa kuwa kuna El Nino hivi karibuni na watu wamepewa ushauri wahamie sehemu za juu ili kuzuia maangamizi. Usipoenda, utaangamia. Vile vile, hata wale waalimu wakiona maisha yao yako hatarini wanapaswa kuambia Serikali ili watolewe kule. Inajulikana kuwa kuna watu fulani waliyosema kuwa hawafai kuwa sehemu hizo. Sen. Munyi Mundigi aliongea juu ya waalimu ambao washughulikia mambo ya mitihani. Walimu wale wanafanya kazi nzuri sana. Wanasimamia mitihani mikuu. Wasiposhughulikiwa vizuri utapata wanafunzi wamepokea alama zisizo zao kwa sababu walimu hao---"
}