GET /api/v0.1/hansard/entries/1299843/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1299843,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299843/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi niongee kuhusu Mswada huu ulioletwa na Sen. Miraj, Mteule wa Kaunti ya Mombasa. Mswada huu unaoongea kuhusu haki na kuchunga watoto wanaopata mimba au kutungwa mimba wakiwa bado wanaenda shule au wakiwa na miaka midogo. Watoto ambao wanapata mimba huzaa watoto wenzao. Hii sheria tunayotaka kuitunga kwa Seneti hii ni sheria kubwa na ya maana sana. Kaunti ya Tana River tuna shida sana. Sisi tunaofanya kazi ya Sheria, pale kortini, tunakutana na dhuluma za watoto wadogo wanao pachikwa mimba katika hali ya kutatanisha, ilhali wao bado wanaenda shule. Katika kaunti yangu, mtoto anayepachikwa mimba, kuna mazungumzo ambayo wazazi wanafanya ili kumaliza yale maneno kinyumbani. Sisi ambao tumeenda kortini mara nyingi tunaona dhuluma kwa watoto hawa waliodhulumiwa. Tena kuna tabia ya kujaribu kuyamaliza haya maneno kinyumbani."
}