GET /api/v0.1/hansard/entries/1299845/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1299845,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299845/?format=api",
"text_counter": 307,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Unapata msichana mdogo amepachikwa mimba. Ametoka shule na maisha yake yashaa haribika. Kisha, kuna mazungumzo ambayo yanafanywa ili watu wajaribu kujiokoa. Hii sheria imekuja kuelezea vizuri sana kwamba, ikiwa ni mtu mzima amejihusisha na kuhadaa watoto na kuwapachika mimba, mambo ya maslaha hakuna tena Kenya. Tunataka hii sheria tuipitishe ili zile mila zinazo umiza wasichana wetu wadogo tuzimalize na tuziondoe kabisa katika Kenya hii. Iwe tuko tuko Tana River, Nairobi, Mombasa. Kwa hivyo, mimi nasimama kuunga mkono haswa vipengele vinavyosema mtoto akipata mimba, wazazi wasimfiche. Tunataka hao wasichana wetu, hata kama wamepata mimba wakiwa wadogo, wasaidiwe kurudi shuleni. Kesi tunazoziona mara nyingi huwa watoto hawa wanafichwa. Na tunaona sana wazazi ambao watoto wao wamepatwa na hii dhuluma, wanajaribu kuwaficha wale watoto ili wasionekane pale nyumbani heshima ya familia imeshuka. Tunataka hii sheria ipitishwe kwa Bunge la Seneti, ili watoto hawa waendelee na maisha yao hasa ya shule. Ukweli ni kwamba wengi waliopata mimba wakiwa bado ni watoto, tumewaona wakirudi shule. Wameendeleza hali zao za kimaisha na wameweza kuhitimu na wengine wakapata kazi kubwa na mabwana. Sheria hii ilioyoletwa, na Sen. Miraj, tukiipitisha hapa kwa Bunge letu, itakuwa ni heshima kubwa kwa mtoto wa kike. Lile jambo lingefaa tuangalie katika sheria hii, ni kuipiga msasa ili isigongane na sheria zingine ambazo tayari zipo katika haki za watoto. Kuna sheria kubwa tunayoiita Children’s Act. Mimi kama wakili, nimekwisha"
}