GET /api/v0.1/hansard/entries/1299847/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1299847,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299847/?format=api",
"text_counter": 309,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na hii sheria. Kati ya maneno ambayo sheria hii imetaja wakati nilisikia ikoongolewa na Sen. Miraj, kuna maneno ambayo nimeona yako tayari katika Sheria ya Watoto. Hivyo basi, wakati sheria hii itapoanza kujadiliwa kwa kina, na kwenda kwa Kamati husika katika Bunge letu la Seneti, tungependa sana ipigwe msasa ili kusiingilie kazi ya kuregelea ama kitu kinachogonganisha na sheria iliyopo. Sheria ya Watoto iko na mambo mengi yanayosaidia watoto na yamebadilisha shida ambazo watoto walikuwa wakipata na kuleta mazuri mengi. Kwa hivyo, ninamuomba, Sen. Miraj, wakati ambao anaendeleza hii sheria, pia aangalie mawazo ya Kamati husika, awasikize ili wapige msasa sheria hii inayoletwa sasa ili ikuwe nzuri. Kwa jumla, hii ni sheria nzuri. Tunaomba sana Maseneta wenzetu waiangalie na waiunge mkono kwa roho moja. Hii ni kwa sababu watoto wetu wasichana ni lazima tuwatetee. Sisi wengine tumezaa watoto wa kike. Leo wako nyumbani. Kesho hatujui itakuwa namna gani. Leo wako nyumbani. Wakienda shule, hatujui kunakuwa namna gani. Ndio tunawafundisha na kuwaambia lakini, majambazi wapo huko nje. Tunakata kuwekwe sheria kali zaidi ya kuchunga watoto wetu wa kike kwa sababu wao ndio maisha yetu ya mbele. Kwa hayo mengi, naunga mkono Mswada huu. Nampa Sen. Miraj kongole kwa kazi aliyoifanya. Tunaomba hii Sheria tuipatie uungaji mkono wa hali ya juu. Asante Bi. Spika wa Muda."
}