GET /api/v0.1/hansard/entries/1299957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1299957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299957/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Mambo ardhi imekuwa ni donda sugu katika Jamhuri yetu ya Kenya. Ninaungana na hawa ndugu zetu wa Mwabundusi kwa kusema ya kwamba mashamba yao yamenyakuliwa au kuchukuliwa. Kulingana na ardhilhali yao, wanasema ya kwamba shirika hili la serikali lilikuwa limepewa zaidi ya ekari 83, halafu sasa wakaongeza mpaka hekari 300. Bw. Spika, jambo hili ni la kuvunja moyo sana kwa sababu nchi hii ya Kenya ni yetu. Hakuna vile wananchi walalahoi watasukumwa katika nchi yao na kupelekwa katika sehemu ambazo wanakaa kwa shida nyingi. Bw. Spika, sio ardhilhali pekee yake. Katika Seneti hii, ninawashukuru kwa sababu wameona kwamba wakileta ardhilhali yao katika Seneti, itashughulikiwa ipasavyo. Sina shaka Kamati ambayo inaongozwa na Sen. Methu, watalishughulikia shida hiyo kwa kidharura ndio wapate suluhu la kudumu. Laikipia pia ina hiyo shida kuhusu watu ambao wamefurushwa kutoka mahali ambapo walikuwa wakiishi. Wanaitwa Marmanet Evictees . Wanaishi maisha ya uchochole na shida ilhali wameleta ardhilhali yao hapa na ikasemekana ya kwamba Kamati iliyoishughulikia ilitoa mwelekeo. Kamati hiyo ilisema kwamba Serikali tayari inapaswa kuwafidia. Kwa hivyo, bila kupoteza wakati, ningependa kusema ya kwamba Kamati ambayo itashughulikia hili swala ni muhimu wapate jawabu ya kudumu. Wakipata jawabu, haitoshi kwa sababu wanatoa mapendekezo ambayo yanabaki kuwa mapendekezo tu. Hayatiliwi mkazo ili yaweze kutekelezwa. Kwa hivyo, mimi naunga mkono hii ardhilhali. Naomba Kamati itakayokabidhiwa iishughulikie. Tukipata mapendekezo, basi yashughulikiwe."
}