GET /api/v0.1/hansard/entries/1299975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1299975,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299975/?format=api",
"text_counter": 73,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa kunipa fursa hii kuchangia ardhilhali ambayo imeletwa na wakaazi wa maeneo ya Kaunti ya Kisii. Wanalalamika kwa sababu ya kunyakuliwa kwa ardhi yao ya jadi na taasisi ya KARI na Kisii Farmers Training Center (FTC). Haya ni masikitiko kwa sababu watu walitoa ardhi kwa taasisi ya Serikali lakini taasisi imemiliki ardhi yote ya jamii hii. Hii ni sawa na kumkaribisha ngamia nyumbani kwako alafu akakutoa ndani ya nyumba. Nimeona katika maelezo kwamba walienda katika Tume ya Ardhi ya Kitaifa mwaka wa 2005. Lakini, karibu miaka minane baadaye, hawajapata suluhu ya swala hili. Nawapongeza kwa kuwa na imani kwamba Seneti itaangalia mambo yao ili dhulma ambazo wamefanyiwa zimewekwa kikomo. Bw. Spika, hata wakati wa ukoloni, ardhi zetu zilichukuliwa vile. Tunaanza kidogo baadaye mnaelezwa kuwa hamfai kuishi pale na ardhi inaenda hivyo kiholela. Baadaye, ardhi inapewa mabwenyenye wanaoanza kufanya biashara na ukulima na mambo kama hayo. Mwaka 2021, kulikuja ardhilhali kama hii ya jamii ya Wajomvu kutoka Kaunti ya Mombasa. Licha ya kupea pendekezo Tume ya Ardhi ya Kitaifa kuingilia jambo lile, mpaka sasa, hawaja ita mkutano wala kukaa kulifuatilia jambo hili. Kwa hivyo, maswala haya yajadiliwe na Bunge ili itoe mapendekezo na ni lazima yatekelezwe. Haina faida watu walete malalamiko yao katika Bunge hili la Seneti na litoe kauli, lakini baadaye zikaliwe na wahusika katika Serikali."
}