GET /api/v0.1/hansard/entries/1299987/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1299987,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299987/?format=api",
    "text_counter": 85,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa nafasi hii. Kuna mchakato ambao unaendelea wa shamba na watu kufurushwa kutoka mashamba yao asilia. Uchunguzi wangu kupitia vyombo vya habari ni kwamba, awamu ya matumizi ya shamba hilo ilitamatika na shamba hilo lilipaswa kurejeshewa wahusika ambao ni wazao wa eneo hilo. Haya ndiyo maswali ambayo watu wa Kaunti ya Kisii wanauliza. Iwapo makataa ya muda wa matumizi ya shamba hili yametamatika, ni jambo la busara mashamba haya yarejeshewe wenyeji kwa sababu wametumia kwa miaka mingi. Miaka iliyoliwa na nzige lazima irudishwe."
}