GET /api/v0.1/hansard/entries/1299989/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1299989,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1299989/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Watu kuishi kama kwamba si wakenya, na wanafahamu urithi wao uko wapi lakini wanasimamiwa na askari kwa mitutu ya bunduki kufurushwa katika mashamba yao, sio jambo ambalo tutakubali. Tunaomba Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili ichunguze ni mashamba yepi ambayo yaliwachiliwa na watu wa maeneo husika ambayo serikali imechukua. Ili iwapo awamu hizo zimekwisha hatua Madhubuti zichukuliwe ili wahusika ama wenyeji wa maeneo haya wapewe mashamba yao. Haya maswala yako kwenye Bunge la Seneti kwa sababu, tumeyaona pia kwenye maeneo ya misitu ya Kakamega na Kaunti ya Migori. Wakaaji wa Kaunti ya Kisii wamewasilisha Ardhihali hii. Tunaomba kwamba haya maswala yashughulikiwe kwa haraka. Asante, Bw. Spika."
}