GET /api/v0.1/hansard/entries/1300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1300,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1300/?format=api",
    "text_counter": 290,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Watu wanaoishi katika vitongoji vya Nairobi wana shida nyingi sana. Hawana makao maalum na hawamiliki ardhi yoyote. Ni muhimu sana kwa Serikali yetu kuheshimu haki za watu wake. Wengi wao wanaishi katika vitongoji duni visivyo na huduma za kawaida kama vile maji, umeme na vyoo. Chini ya Katiba yetu watu hawa wana haki sawa na wananchi wengi wa taifa hili. Hawa walichangia pakubwa kuweka Serikali hii kupitia kwa kura zao. Hata hivyo, wanadhulumiwa kwa sababu wao ni wanyonge."
}