GET /api/v0.1/hansard/entries/1300371/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1300371,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1300371/?format=api",
"text_counter": 469,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Pia nami ninaunga mkono hii Hoja iliyoletwa hapa mbele na Seneta ambaye pia ni Kamishna. Kwanza ni kwamba, hii Kamati ya majadiliano ambayo inaendelea hivi sasa ni muhimu sana kwa taifa na kwa kila Mkenya. Hii ni kwa sababu imeweza kuleta amani na kufanya nchi ikatuliwa, kisha watu wakawa wanaendelea na mambo yao kama kawaida. Kitu cha kwanza ambacho nataka hii Kamati iweze kufanya ni kwamba iangalie haki ya mwananchi. Sio haki ya polisi pekee yake. Nazungumza kuhusu haki ya wananchi kwa sababu wananchi wengi wanashikwa kiholela bila sababu na kubandikiwa mashtaka. Ni muhumu kuwe na kitu mwafaka ambacho kitawekwa katika kipengele cha sheria kuona ya kwamba wengi wao ambao wanashikwa, kutakuwa na hali nzuri ya kushikwa kwa heshima. Pia ukitaka kushikwa kama mweshimiwa au kama mimi Seneta hivyo ndivyo mtu yeyote yule atashikwa. Kamati hii yenye Uelewano ambayo hivi sasa iko katika mazungumzo haya, iweze kuona ya kwamba, kama mimi ukiniagiza niende katika kituao cha polisi mahali fulani nitakwenda. Hata hivyo, utapata ya kwamba hata waheshimiwa pia hawaheshimiki sasa. Katika macho ya Wananchi, wakiona kwamba waheshimiwa wao hawa heshimiki hata na askari, inakuwa jambo la aibu. Jana mimi mwenyewe nilikuwa kule Mavoko na tulienda na wale vigogo wetu wa kuu katika mirengo ya siasa. Hata baada ya kuwaeleza ya kwamba tunapeleka chakula na tunaenda kuwaona wale watu ambao wameathirika hatukuruhusiwa. Hata kama kuna amri, lakini ingekuwa vyema kungekuwa na heshima, kwa sababu wale walikuwa ni viongozi waliowaambia wale askari ya kwamba hakungekuwa na fujo kwa sababu walikuwa wanapeleka chakula na tungeongea vizuri na wananchi. Ninaunga mkono Kamati hii iongezwe muda ule ambao wamesema wana haja ya kuupata ili waweze kutengeneza ripoti nzuri. Hiyo ripoti ndio itakuwa ngao na ulinzi wa umoja wetu katika Kenya. Naunga mkono."
}