GET /api/v0.1/hansard/entries/1302/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1302,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1302/?format=api",
    "text_counter": 292,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 398,
        "legal_name": "Yusuf Hassan Abdi",
        "slug": "yusuf-hassan-abdi"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, ni jambo la kusikitisha kuona Serikali yetu ikitumia nguvu dhidi ya maskini hohe hahe na kubomoa nyumba zao na bila kujali maslahi yao. Waliotekeleza kazi hii walionyesha unyama na ukatili wa kupindukia. Hawakujali hali ya maisha ya watu wa kawaida, akina mama na watoto. Kwa nini Serikali hii haijali maslahi ya wananchi maskini? Kama kweli inajali maslahi ya watu wake, kwa nini ichukue hatua ambazo kila wakati zinaumiza mwananchi wa kawaida? Ni muhimu Serikali yetu ichukue hatua za dharura kurekebisha makosa yaliyofanyika. Ingawa Hoja hii haijishughulishi na maisha ya watu wa kawaida, kuna watu wengi walioachwa bila makao. Kwa nini Serikali isihudumie watu hawa na kuwapa makao? Wakati huo watu hawa wanalala nje na familia zao. Sote tunajua kuna baridi sana nje. Watu hawa wanateseka sana. Ninaiomba Serikali hii kuiheshimu Katiba yetu inayowapa wananchi wote haki sawa. Ningependa kuishukuru Kamati hii kwa maoni yake kuwa watu wa kitongoji cha Kiambiu wana haki kuwa pale na wasitimuliwe bila kupatiwa makao mapya na Serikali hii. Mimi kama mhe. Mbunge wa Eneo la Kamukunji ninakubaliana na maoni haya. Wakati umefika kwa sisi kutunga sheria zitakazolinda haki za watu maskini wa jiji hili na wale wengine waliobomolewa nyumba zao. Ni muhimu kama vile Hoja hii inavyopendekeza Serikali iwafidie walioathirika kwa kuwapa ardhi ambapo watajenga nyumba zao upya. Hii ni kwa sababu walitumia mali na rasimali zao kujenga nyumba zilizombolewa. Bi. Naibu Spika wa Muda, Wakenya wengi wanaoishi nje ya nchi hii wangependa kuleta rasilimali zao hapa ili kuinua uchumi wetu. Lakini haya yatawezakanaje ikiwa wanaona kwenye runinga zetu matingatinga ya Serikali yakibomoa nyumba za watu wake? Je, watakubali kuja kuwekeza mali yao hapa? Ni muhimu kwa sisi kuwatia moyo Wakenya hawa ili wawezekuleta pesa zao hapa ili tuimarishe uchumi wetu na tuwe na maendeleo mengi hapa nchini."
}