GET /api/v0.1/hansard/entries/1304359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1304359,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1304359/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Nimesimama hapa kimasomaso, mchana peupe, kupinga Hoja hii iliyoletwa na Mratibu wa walio Wachache katika Seneti. Sisi si jongoo, tunavichwa vyetu na tunaweza kufikiria kibinafsi. Hapa Seneti, Hoja inayofaa kuungwa mkono na pande zote mbili, huletwa na Kiongozi wa Walio Wengi. Hoja hii huungwa mkono na Kiongozi wa Walio Wachache. Leo Hoja imefadhiliwa na Mratibu wa walio Wachache na kuungwa mkono na mdogo wake. Hii inaashiria kuna azimio fiche kwenye tendo hili."
}