GET /api/v0.1/hansard/entries/1304361/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1304361,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1304361/?format=api",
    "text_counter": 224,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Maseneta vijana katika Seneti wanafaa kupewa nafasi ya kusikiza, ‘kunusa,’ ‘kuonja’ na kusoma Hoja inayoletwa katika Seneti. Ukiangalia orodha ya Maseneta ambao inapendekezwa waunde Kamati, katika upande wa walio wengi, ni wale ambao walikuwa wakati Gavana wa Meru aliletwa hapa Seneti mara ya kwanza. Hii inanyima nafasi Maseneta wengi vijana walio katika upande wa walio wengi. Hoja iletwe kwenye kikao cha Seneti. Sitakubaliana na maoni kuwa wakati Gavana ataletwa kwenye kikao cha Seneti, hatasikizwa. Kwenye Bunge la Kaunti la Meru, Wawakilishi Wadi 59 walisikiza na wakapitisha Hoja. Naomba Maseneta wa upande wa walio wengi tusifuate mkondo kama samaki aliyekufa. Hoja iletwe kwenye kikao cha Seneti ili sisi sote tusikize, tuchangie na kufanya maamuzi mbele ya Wakenya wote. Asante sana, Bw. Spika. Napinga Hoja hii."
}