GET /api/v0.1/hansard/entries/1304371/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1304371,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1304371/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja hii. Kubanduliwa mamlakani kwa gavana kwa kupitia njia ya impeachment ni jambo muhimu sana ambalo linatoa matatizo makubwa kwa yule ambaye anabanduliwa. Hii ni kwa sababu ukibanduliwa mamlakani, ina maana kwamba, huwezi kukaa katika ofisi ya umma kwa kazi yoyote ile ambayo una nia ya kuifanya. Kwa hivyo, ni lazima tumpe yule mhusika nafasi nzuri ya kuweza kujitetea kutokana na mashtaka ambayo yanamkabili. Njia ya kamati ni mwafaka kabisa ambayo inampa mhusika nafasi nzuri ya kujitetea na kusikiza yale mashtaka ambayo yataletwa mbele yake. Ijapokuwa kikao cha Seneti nzima kina nafasi sawa na kamati, tumeona katika historia ya impeachment ya waheshimiwa Sonko na Waititu, hawakupata fursa nzuri ya kujieleza. Hii ni kwa sababu kazi yenyewe ni nyingi na inatakiwa ifanyike kwa muda wa siku mbili. Wiki iliyopita, Mawaziri wawili walirudi kwa vile hatukuwa na quorum katika Bunge hili. Tukikaa hapa siku ambayo itatakikana tukae, tunajua mara nyingi, Maseneta huchelewa kufika katika Bunge hili asubuhi. Kwa hivyo, itakuwa ni aibu kwamba wale ambao wataamua kesi hawako mahakamani lakini kesi inaendelea kusikizwa bila wao. Naona njia mwafaka ni kuwa na Kamati. Wale ambao watachaguliwa katika Kamati ni Maseneta kama Maseneta wengine. Hii kadhia ya kubandikia Kamati masuala ambayo hayako, kwa mfano, tuhuma za kupokea hongo ama kufanya kazi kimapendeleo, haifai. Hii ni kwa sababu Seneta yeyote ambaye anahudumu katika Kamati ni Seneta kama Seneta mwingine. Kamati zote zinapokaa, ni kamati za Seneti. Kwa hivyo, kawaida zote za kuhakikisha kwamba haki na usawa zinafanyika. Bw. Spika, nafasi ya kamati itakuwa ndio njia bora kabisa ya kuweza kusikiza madai ambayo yamependekezwa na Bunge la Kaunti ya Meru. Itawapa fursa na nafasi sawa watu wote; Wabunge wa Kaunti ya Meru na Gavana Kawira Mwangaza, kuweza kusikiza kesi ile na kutoa uamuzi ambao utasaidia kuleta haki na usawa. Hatuwezi kuwa kama Seneti hapa ---"
}