GET /api/v0.1/hansard/entries/1304422/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1304422,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1304422/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa wakati huu kuchangia. Wakati gavana huyu alikuwa hapa kujitetea alipoletwa na kaunti yake husika, aliponea chupuchupu. Utetezi wake ulifanywa katika kikao ambacho hatukuwepo lakini kwa sababu ya uamuzi wa jumla wa Seneti kwamba waliyokubaliana nayo pia sisi tukubali, tukakubali shingo upande. Watu wa kaunti hii wana mambo ambayo wangependa kusikia yakitajwa, yakijadiliwa na yakizungumziwa peupe mchana. Pia wanataka kujua rafiki yao ni nani na asiyekuwa rafiki yao ni nani. Wanataka kujua kama Seneti inajua yanayoendelea katika kaunti yao ama hapana. Wanajua kwamba katika majadiliano ya watu wachache, kuna mazungumzo ya chini kwa chini ambayo hao hawahusiki. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}