GET /api/v0.1/hansard/entries/1305247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1305247,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1305247/?format=api",
    "text_counter": 225,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hoja ya pili, Bi. Spika wa Muda. Nimesimama kwa mujibu wa Kanuni ya Kudumu Nambari 53(1) kuomba Kauli kutoka kwa Kamati ya Kudumu ya Barabara, Uchukuzi na Makao kuhusu hali ya ujenzi wa barabara pacha kutoka makutano ya Sang’alo hadi Kanduyi katika Kaunti ya Bungoma. Katika kauli hiyo, Kamati iangazie yafuatayo- (1) Iwasilishe hati zote za zabuni kutoka Serikali ya Kaunti ya Bungoma zilizotumika katika ujenzi wa barabara hiyo, ikiorodhesha vifaa vyote na gharama zote pamoja na gharama ya wafanyikazi waliyohusika katika ujenzi wa barabara hiyo. (2) Iwasilishe nakala ya makubaliano kati ya Serikali ya Kitaifa na Serikali ya Kaunti ya Bungoma kuhusu mradi huo, ikielezea kwa kina kazi inayoendelea na iwapo muda uliokadiriwa kukamilika kwa mradi huo ulipita. (3) Iarifu Seneti hali halisi ya kifedha ya mradi huo, ikielezea kiwango cha fedha kilicholipwa na Serikali ya Kitaifa kwa Serikali ya Kaunti ya Bungoma na sababu zinazopelekea kucheleweshwa kwa malipo ya fedha zilizosalia. Asante, Mhe. Spika wa Muda."
}