GET /api/v0.1/hansard/entries/1315951/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1315951,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1315951/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taita Taveta County, UDA",
"speaker_title": "Hon. Haika Mizighi",
"speaker": null,
"content": "ambao wanawatazamia sana kwa msaada mmoja ama mwingine. Tafadhali wakifika kule waweze kuwatambua Wakenya walioko kule waweze kuwaskiza na kuwahudumia kwa hali ambayo ni ya sawa. Tumeona Wakenya wengi wakipata changamoto nyingi wakiwa kule nje ya nchi, wengine wameenda kimasomo, wengine wameenda kikazi na wananyanyasika kule ilhali tunao mabalozi ambao wako kule wanaostahili kuwasaidia. Ni jukumu lao. Ninataka pia kuwaeleza wakiwa kule nje ya nchi kuwa wao ni macho ya nchi. Vile vile, wanasomwa kama waakilishi wa nchi, na ni vyema waweze kujibeba kizalendo kwa kupeperusha bendera yetu ya Kenya juu na kuweza pia kuangalia nafasi nyingi ambazo zinaweza kuboresha nchi yetu, kama vile nafasi za kazi na biashara, na pia kuuza nchi yetu kwa zile nchi nyingine kwa mambo ya utalii na mengine kama hayo. Ninachukua fursa hii pia kumpongeza Rais kwa uteuzi wake ambayo ameufanya kwa uangalifu kabisa. Tumeona idadi ya wanawake walioteuliwa ikiwa nzuri kabisa, wakiwa wanawake kumi, na pia tumeona ameweka idadi ya wanaume kisawasawa. Vile vile, ameangalia sehemu mbalimbali na utendakazi wa hao mabalozi. Tunamjua vizuri Balozi Mama Betty Cherwon ambaye anapelekwa kule Ufaransa. Ni mama ambaye ana ueledi sana wa mambo ya kidiplomasia. Ningependa pia kumpongeza dada Janet Oben Mwawasi ambaye anatoka Kaunti ya Taita Taveta. Hata yeye amepata fursa ya kuwa balozi wa kule Rwanda. Ninampa kongole sana. Asante Spika wa Muda kwa kunipatia hii fursa ili kuchangia Ripoti hii. Ninaunga mkono. Asante sana"
}