GET /api/v0.1/hansard/entries/1319677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1319677,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1319677/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda. Ningependa nami nitoe sauti yangu kuhusu Hotuba ya Rais aliyotoa hivi majuzi. Kuanzia wakati nilipokuwa mtoto mpaka umri huu ambao nimefika, katika mila na desturi za Wakenya, Rais anapotaka kutoa hotuba, huwa sote tuko juu juu. Raha huwa ziko juu na kila mtu hutaka kusikia ni maneno gani au mipango ipi aliyo nayo Rais kwa nchi yetu. Cha kustaajabisha ni kuwa, katika Hotuba aliyotoa Rais juzi, watu wengi walikuwa hawana interest ya kuisikiza kwa sababu maneno ambayo tulielezwa katika Bunge la Taifa ni yale yale maneno ambayo Wakenya husikia kila siku wamuonapo Rais amesimama juu ya gari akiwahutubia watu barabarani. Hiyo ndiyo maana sijaona tofauti ya yale maneno ambayo sisi husikia mitaani na yale ambayo Rais alizungumza katika Hotuba yake."
}