GET /api/v0.1/hansard/entries/1319678/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1319678,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1319678/?format=api",
"text_counter": 294,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
"speaker": null,
"content": "La pili, Mhe. Spika wa Muda, ni mengi ambayo Rais alizungumzia. Kuna mazuri hapo ndani. Vile vile, ni lazima tukashifu pale ambapo tunaona kuna mambo ambayo hayako sawa. Kitu ambacho nitaunga wenzangu mkono ni kuhusu hili suala la Hustler Fund. Imenishangaza na mpaka dakika hii, nimepigwa na butwaa kusikia kwamba kuna mtu amepata Ksh4,500,000. Labda, ningepata namba ya simu ya huyo mtu ili nihakikishe kwa sababu sitaki kuita mtu mwongo. Hii Kenya tunayoishi, dakika hii, mtu yeyote anayeweza kupata Ksh4,500,000 kwa kupitia Hustler Fund, nina hakika habari ingekuwa imesambaa katika mitandao yote na kila mtu angekuwa ameiona. Ninataka kuhakikisha tu. Sijaita mtu mwongo."
}