GET /api/v0.1/hansard/entries/1319680/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1319680,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1319680/?format=api",
    "text_counter": 296,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Malindi, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Amina Mnyazi",
    "speaker": null,
    "content": "Kitu kingine ambacho ningependelea kiweze kuongelewa zaidi ni kuhusu gharama ya maisha. Hili sasa ni donda sugu katika Kenya yetu. Hili ni jambo ambalo tumelizungumza na kulikariri zaidi ya mara moja. Sikusikia jambo lolote kuhusu mafuta yetu kushukishwa bei. Sasa hapo ndipo donda sugu la matatizo ya Kenya yanapoanza. Sijasikia chochote kuhusu stima na kama itashukishwa bei. Tukisema gharama ya maisha imepanda, hatumaanishi kwamba ni unga wa sima peke yake. Tunamaanisha bei ya chakula, stima, maji na karo ya watoto wetu shuleni iweze kushukishwa. Kwa hivyo, kama Hotuba ya Rais ingekuwa imeangazia zaidi kuhusu masuala ya mafuta, maji na stima, ningekuwa mtu mwenye furaha kabisa."
}